SERIKALI imeendelea kupaa katika ukusanyaji wa mapato baada ya
kukusanya hadi Sh trilioni 1.79, ambazo imezipeleka katika huduma za
jamii, ikiwamo elimu, maji, miundombinu na miradi ya maendeleo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile
alisema
hayo jana wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi
cha Februari mwaka huu. Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Alphayo Kidata alisema makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2
Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.
Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900
kwa mwezi. Dk Likwelile alitaja maeneo ambayo fedha hizo zimeelekezwa ni
kwa Mamlaka ya Elimu (TEA) iliyopewa Sh bilioni 23.078; Sh bilioni 18.7
zinatekeleza utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali,
msingi hadi kidato cha nne kwa ajili ya ada, chakula na ruzuku.
Aidha, Sh bilioni 13 zimeelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu na Sh
bilioni moja zitatumika kujengea uwezo walimu walio masomoni na
wakufunzi wao. Pia Sh bilioni mbili zimeelekezwa kupanua udahili katika
mkoa wa Dar es Salaam kama Rais John Magufuli alivyoahidi katika mkutano
wake na wazee wa mkoa huo.
Dk Likwelile alitaja maeneo mengine yaliyonufaika na fedha hizo na
shilingi kwenye mabano ni Mpango wa Maji Vijijini (bilioni 17.1),
maendeleo ya ujenzi wa barabara (bilioni 58.8), miradi ya umeme vijijini
(bilioni 20.2), reli (bilioni 2.034) Serikali za Mitaa (bilioni 4.5),
na Mahakama zimepatiwa Sh bilioni 12.3.
Wakati huo huo imeelezwa kuwa makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.
Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900
kwa mwezi. Aidha, Dk Likwelile alisema ili kuwajengea uwezo walimu walio
masomoni na wakufunzi wao, Wizara imetoa Sh bilioni 1.65 kwa ajili ya
mafunzo kwa vitendo.
Kati ya fedha hizo, wakufunzi wamepatiwa Sh milioni 431.6, walimu
walio masomoni wametengewa Sh milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya
kufundishia, posho na nauli.
Alisema kuwa fedha nyingine kati ya hizo, kiasi cha Sh bilioni 573.7
zimetolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa umma na ulipaji wa
deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa Sh bilioni 842.1 na mifuko ya
hifadhi za jamii Sh bilioni 81.13.
Aidha kiasi kilichotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za
maendeleo ni Sh bilioni 166.2 huku Chuo kipya cha Sayansi ya Tiba
kilicho katika hatua ya ujenzi cha Mloganzila huko Kibamba, nje ya Jiji
la Dar es Salaam, kimepatiwa Sh bilioni 18 .
0 comments:
Post a Comment