Dar es Salaam, Februari 2, 2016-
Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya
kidijitali imetangaza huduma ya bure ya WhatsApp kwa watumiaji wa huduma
hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kutoa ofa ya
bure ya mtandao huo wa jamii nchini.
bure ya mtandao huo wa jamii nchini.
Akitangaza
upatikanaji bure wa huduma hiyo kwa vyombo vya habarijijini Dar es
Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kuwa wateja wote wa
Tigo wanaotumia vifurushi vya intaneti vya kampuni hiyo kwa wiki na
mwezi watapata huduma ya WhatsApp bure. Tigo ina wateja zaidi ya
milioni 10.
Huduma
ya WhatsApp ambayo ni maarufu kwenye kutuma ujumbe kwa njia ya simu,
ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania na duniani
inatumiwa na watu wapatao milioni 900. WhatsApp inawezesha watumiaji
kubadilishana habari, ujumbe, video na miito ya sauti.
“Kuanzia
sasa na kuendelea wateja wote wa Tigo wanaonunua vifurushi vyetu vya
wiki au mwezi watakuwa na fursa ya kufurahia WhatsApp BURE. Hili
linawezekana kama mteja ana smartphone. Huduma ya bure ya WhatsApp kwa
wateja wetu inaonesha jinsi tulivyojikita katika kuboresha mabadiliko
kwenye maisha ya kidijitali na hivyo kuongoza kwenye kutoa teknolojia
ya hali ya juu pamoja na ubunifu”, alisema Gutierrez.
Kwa
Mujibu wa Gutierrez, ili kufurahia huduma hii, jambo analohitaji mteja
wa Tigo ni kuwa na kifurushi cha intaneti cha wiki au mwezi ambacho
anaweza kukipata kupitia *148*00# à Tigo-Tigo Xtreme/MiniKabangà Wiki
au Mwezi + WHATSAPP YA BURE. Huduma hii inapatikana kwa wanaomiliki
simu za aina ya Blackberry, Android na Nokia Symbian60.
WhatsApp
ni huduma dada na huduma huduma Facebook ambayo iliingia makubaliano na
Tigo mwaka 2014 na kuwapa fursa wateja wa Tigo huduma ya Facebook bure
na kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao.
0 comments:
Post a Comment