Mara nyingi tumekua tukiona au kukutana na watu au ndugu
zetu wanaojiita wawakilishi wakijaribu kutushawishi kuingia katika kile
wanachokiita biashara zenye mafanikio, ambapo wanatushawishi kujiunga na
kampuni inayouza bidhaa zake kwa
mfumo wa Network Marketing au
Multi-Level Marketing (MLM). Katika mfumo huu unapata commission na
faida kwa kuingiza watu wengine wanunue bidhaa husika na faida yako
itaendelea kua kubwa kama na wao watashawishi watu wengine wajiunge
katika msururu huu. Makampuni haya kwa hapa Tanzania yapo mengi wakiuza
bidhaa kama za Aloevera, Kahawa zenye mchanganyiko wa Garnodema n.k.
Naomba itambulike kua Lengo la uzi huu sio kukosoa kampuni
yeyote ile, bali ni kueleza na kuelimisha umma athari za mfumo wa
kilaghai unaotumika katika biashara za namna hiyo
Kabla sijaamua kuandika uzi huu nimekua nikiona watu wengi
wakidanganyika na kuingizwa mkenge kwenye biashara hizi aidha kwa
kutokujua ama kuingizwa tamaa kwa ushawishi wa wawakilishi hawa ambao
wanakua na vipeperushi vinavyotoa maelezo ya biashara huku vikionyesha
baadhi ya watu waliofanikiwa katika mfumo huu wakiwa katika picha na
Magari Mazuri na Majumba ya Kifahari.
Network Marketing au MLM ni mfumo unaofanya kazi kwa Idea
kwamba unauza bidhaa kwa watui ambao nao watauza bidhaa kwa watu ambao
nao watiuza. Mfumo huu kamwe hauwezi kusemwa kua ni mpya kwenye masoko
ili upate msamaha wa kutokuhusianishwa na kanuni na taratibu za kawaida
za Marketing katika uuzaji na ununuzi wa bidhaa. Mfumo huu una ulaghai
wa hali ya juu na kiuhalisia Mfumo mzima hauna faida hasa kwa watu wa
chini, na sio sustainable kwa muda mrefu - in reality the system ‘is
designed to fail”
Swali ambalo ningependa ujiulize ni hili; Kama bidhaa
husika ni nzuri sana na inahitajika katika jamii kama wanavyoinadi,
kwanini wasitumie mfumo wa kawaida wa masoko ambao umeinufaisha dunia
nzima tangu karne?. Jambo la kwanza kabisa ambalo mtu yeyote lazima
alielewe ni hili; Katika biashara yeyote swala la demand and supply au
kwa Kiswahili Ugavi na mahitaji lazima lizingatiwe na kama ukakosea
ukafanya makadirio ya chini au ya juu sana katika kimojawapo kati ya
hivyo basi hakuna mafanikio yeyote yatakayo patikana katika biashara
utakayoianzisha. MLM nyingi zinaoverestimate supply and demand kwa
kiwango cha juu sana, Na tatizo kubwa hapa ni la kutokutumia akili ya
kawaida kabisa; Kivipi sasa?.
Chukulia mfano huu; Tuseme wewe ni mwakilishi wa mojawapo
ya makampuni haya na ukaweza kuwashawishi wenzio (wauzaji) kumi ukapata
commission na faida kiasi ambao watadhamini kumi na wao kudhamini
wengine kumi kila mmoja, mpaka kufikia kizazi cha tatu utakua na idadi
ya watu 1000, na hapo utakua umeumaliza mtaa wako. Kufikia kizazi cha
sita utakua umefikisha watu 1,000,000 na huo utakua ni mkoa mzima tayari
na kila mmoja katika hawa akiamini katika mafanikio yatakayotokana na
uuzaji wa bidhaa husika, lakini watamuuzia nani sasa na kila mmoja ni
muuzaji?. Kwenye vikao vyao utawasikia “Kila mmoja hapa anaweza, hii ni
fursa ya maisha, angalia mahesabu utaniamini”, ila Jaribu kuongelea
kuhusu oversaturation ya soko na hasara itakayosababishwa nayo
utawasikia wakikuambia “sio kwako bwana mafanikio haitatokea hivyo kwako
nayaona mafanikio yako hata nikikuangalia machoni”. Tumia akili ya
kawaida utapata jibu kuhusu hilo.
Network Marketing ni mfumo wa kiunyonyaji katika mahusianao
ya mtu na Kama uko katika biashara hii lazima ukubali kumeza ukweli
mgumu kwamba biashara yako inakua kutokana na exploitation of personal
relationships. Baada ya kuingia katika biashara hii, marafiki na ndugu
zako wanakua ni wateja wako, sasa jiulize uko tayari kumwingiza Mama
yako kwenye huu mfumo wa wizi ukijua hakuna faida kubwa mbeleni?
Kufeli kwa biashara yeyote ile kunaumiza sana, ila kwa
biashara yeyote ndogo kunakuwepo japo nafasi ya kufanikiwa. Nafasi hiyo
ndogo ya mafanikio kamwe haipo kwenye MLM labda kama faida inayotokana
na kushindwa kwa wengine utaitafsiri kama mafanikio.
0 comments:
Post a Comment