Wizara ya afya kuanzia leo 24 Desemba 2015 imepiga marufuku matangazo
yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na
mitandao ya kijamii.
Kwa wale wenye vibali wanatakiwa kuviwasilisha vibali
na matangazo yao
kwenye Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.
Utoaji wa elimu ya afya kwa umme unaofanywa na watoa huduma za tiba
asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii
umepigwa marufuku hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.
Watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini kote wanaagizwa
wawasilishe kwenye Baraza nyaraka zote muhimu ndani ya wiki mbili
kuanzia leo Desemba 2015. Baadhi ya nyaraka hizo ni zile zinazohusu
kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za kumiliki mashine
zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili na tiba mbadala
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku
14 kuanzia leo 24 Desemba 2015, lipitie nyaraka zote zikapowasilishwa
zinazohusu usajili wa watoa huduma, usajili wa vituo vyao, ikiwa ni
pamoja na maduka ya dawa za asili na dawa za tiba mbadala, usajili wa
dawa zote zinazotumika katika huduma hizo na usajili wa mashine zote
zinazotumika katika huduma za tiba asili na tiba mbadala.
Taarifa hiyo imetolewa na Dismas Lyassa kwa niaba ya Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangala
na kusainiwa na M.O John, Kaimu Katibu.
0 comments:
Post a Comment