Jumamosi February 20, 2016 umechezwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Tanzania bara kati ya Yanga vs Simba (Dar es Salaam derby) na
kuishuhudia Yanga ikipata ushindi wa
pilli wa goli 2-0 dhidi ya Simba
kwa mara ya pili kwenye msimu huu.
Mengi yamezungumzwa baada ya mchezo huo lakini huu ni mtazamo wangu baada ya kuufatilia mchezo ho kwa umakini mkubwa .
Kabla ya Abdi Banda kuoneshwa kadi nyekundu na kuiacha Simba ikiwa pungufu kwa mchezaji mmoja hali ya mchezo ilikuwaje?
Kabla ya kadi nyekundu kutolewa kwa Abdi Banda, game ilikuwa ime-balance
na Simba walikuwa wameitawala Yanga kwenye eneo la midfield lakini
baada ya kadi nyekundu ya Banda, ikailazimu Simba kumshusha Majabvi
kwenye nafasi ya ulinzi wa kati. Katika eneo la kiungo wakabaki Ndemla,
Kazimoto na Mkude Yanga wakawa wengi kwenye eneo la katikati.
Kadi nyekundu iliwaathiri kwa kiasi gani wachezaji wa Simba?
Namna ambavyo wachezaji wa Simba walivyochukulia tukio la kutolewa kwa
Abdi Banda iliwashusha morali. Wachezaji wakaona tayari wapo pungufu
kwenye mechi kubwa dhidi ya Yanga halafu kadi imetoka mapema ikawavunja
ari. Lakini kama wachezaji wangeandaliwa kisaikolojia kabla ya mechi
kwamba wanaenda kwenye mechi kubwa, tukio la kadi nyekundu linaweza
kutokea wakati wowote, tukio kama hilo likitokea wanachezaje ingeweza
kuwasaidia.
Je Banda alistahili kadi nyekundu?
Kadi ya kwanza ya njano aliyooneshwa Banda ukiangalia unaweza kudhani
alikuwa ni mtu wa mwisho na kujiuliza kwanini hakupewa straight red
card. Kwasababu watu wengi wanavyoelewa ni kwamba ukicheza rafu ukiwa
mtu wa mwisho unapata red card. Lakini haiko hivyo, kadi ya njano
alistahili. Na nimsifu mwamuzi kwa maamuzi aliyofanya kwa kadi ya
kwanza. Kwasababu hata kama Ngoma angefanikiwa kumpita Banda tayari
kulikuwa na Juuko ambaye angeweza kuokoa mpira kutoka kwa Ngoma. Kadi ya
njano ya kwanza ilikuwa sahihi kabisa.
Kadi ya njano ya pili Banda alistaili bila kujalisha alishapewa kadi ya
njano awali. Kwasababu sheria inasemaje? Kama alifanya makosa inabidi
aadhibiwe kulingana na makosa yake bila kujali kama tayari anakadi au
hana.
Nini kilitakiwa kifanyike baada ya kadi nyekundu ya Banda?
Nilifikiri kocha na benchi lake la ufundi watafanya mabadiliko ya mapema
kwa kumtoa striker mmoja na kumuingiza beki moja au kiungo lakini
kwenye benchi lao hakukuwa na beki. Lakini ili kuweza kumudu ushindani
kwenye eneo la katikati wangemtoa Kiiza au Ajib. Lakini kwa mtazamo
wangu wangemchomoa Kiiza halafu waongeze kiungo kwa ajili ya kuongeza
ushindani kwenye eneo la katikati.
Wakati huo wanamuongezea majukumu Ajib ya kukimbia na kupambana kwenye
eneo la mbele kwasababu aina ya uchezaji wa Ajib angemudu kucheza akiwa
mshambuliaji pekee.
Bila shaka yoyote kadi nyekundu aliyopewa Banda mapema iliwaathiri Simba
kwa kiasi kikubwa kwa dakika zilizokuwa zimesalia kwenye mchezo.
Angalia video hapa chini uone namna Shaffih Dauda na Ally Mayay
‘Tembele’ walivyo dadavua kuhusu kadi nyekundu aliyooneshwa Abdi Banda
0 comments:
Post a Comment