KOCHA wa Simba Jakson Mayanja amemkingia kifua mchezaji wake Ramadhan
Kessy kwa kile kinachodaiwa kuwa alifanya uzembe wa makusudi
ulioigharimu timu yai
hadi kufungwa na Yanga mabao 2-0 kwenye Uwanja wa
tTaifa Jumamosi.
Katika mchezo bao la kwanza lilisababishwa na makosa ya Kessy
aliyekuwa akijaribu kumrudishia mpira kipa wake, Vincent Angban lakini
ukawahiwa na Donald Ngoma na kufunga.
Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakilalamika kuwa huenda Kessy aliuza
mechi ndio maana alifanya uzembe wa makusudi, jambo ambalo Mayanja
alisema kama ni makosa yalitendeka kwa wachezaji wote.
Akizungumza jana Dar es Salaam Mayanja alisema walijiandaa vizuri
dhidi ya Yanga lakini kilichoshangaza wachezaji wake walicheza tofauti
na kile walichoelekezwa.
“Hatuwezi kusema ni Kessy peke yake, wachezaji wote hawakucheza kama
nilivyowaelekeza sijui ni nini kilitokea,”alisema na kuongeza kuwa watu
wamekuwa wakilalamika bila kujua matatizo ya kiufundi.
Mayanja aliwashukuru mashabiki wa Simba kwa kuwaunga mkono katika
mchezo huo huku pia akiwataka kutokata tamaa kwani kuna michezo mingine
ya ligi inakuja.
Alisema kwa sasa anaangalia mbele michezo ijayo katika kuhakikisha inafanya vizuri kama ilivyotokea kwa michezo mingine.
Wakati Mayanja akiongea hayo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
wa Yanga Jerry Muro alimpongeza Kocha huyo kwa kuwa muungwana.
Alisema Mayanja alionyesha uungwana kwa kuwa aliona kuwa wachezaji wake waliteleza na sio kumlaumu mwamuzi au mchezaji.
0 comments:
Post a Comment