Visa vya watu kuuawa vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara Bujumbura
Mwanamziki mmoja kutoka Burundi amepatikana amefariki katika mji mkuu wa
Burundi, Bujumbura baada ya kukamatwa na polisi, hii ni kwa mujibu wa
taarifa kutoka
kwa kundi la wanahabari la SOS.
kwa kundi la wanahabari la SOS.
Taarifa hizo zinasema kwamba mwili wa Pascal Tresor Nshimirimana
ulipatikana Jumamosi eneo la Musaga, karibu na gereza kuu la Bujumbura.
Polisi wanasema Pascal alijaribu kumnyang'anya bunduki afisa wa polisi,
na akauawa na risasi ililofyatuka kutoka kwa bunduki hiyo kwa bahati
mbaya
Bw Nshimirimana alikuwa mmoja wa waandamanaji ambao walipinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza
Katika kisa kingine, mwili wa kiongozi wa vijana William Nimubona ulipatakana katika maeneo ya Kavuma jijini Bujumbura.
Hata hivyo, hakuna taarifa huru za kudhibitisha mauaji ya kiongozi huyo.
Bw Nimubona alikuwa kiongozi wa mrengo wa vijana katika chama cha
National Liberation Forces (NLF) kinachoongozwa na Agathon Rwasa,
kiongozi wa upinzani aliyekubali kuchukua kiti cha naibu wa spika baada
ya Rais Nkurunziza kushinda uchaguzi tata wa muhula wa tatu.
0 comments:
Post a Comment