Rapper 50 Cent amejisalimisha kwa kifungu cha 11 cha sheria ya kufilisika nchini Marekani ili iwe kinga ya kupokonywa mali zake.
Kifungu cha 11 kinayapa muda makampuni kujipanga katika mambo yake
kifedha huku yakilinda dhidi ya matakwa ya wanaowadai. Msanii huyo
ambaye
pia ni mfanyabiashara amewasilisha nyalaka mahakamani
zinazoonesha kuwa ana mali na madeni yanayoanzia dola milioni 10 hadi
50, kwa mujibu wa Wall Street Journal.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya mahakama kuamuru alipe dola
milioni 5 kutokana na kesi ya kuvujisha mkanda wa ngono wa ex wa adui
yake, Rick Ross.
50 Cent alitoa tangazo hilo siku hiyo hiyo aliyotakiwa kupanda kizimbani
kwenye mahakama ya Manhattan kuhusiana na adhabu ya faini aliyopewa.
Mwanamke huyo, Lestonia Leviston alitakiwa kulipwa kiasi hicho cha fedha
kutokana na kuathiriwa kihisia baada ya 50 kupost online sex tape yake
(Leviston) akiwa boyfriend wake wa zamani.
Staa huyo yeye mwenyewe anasikika akiwa kama msimulizi wa video hiyo ya dakika 13 kwa kujipa jina Pimpin’ Curley.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Florida ambaye ana mtoto na
Rick Ross alidai mahakamani kuwa video hiyo ilitaka kumfanya ajiue.
Hata hivyo mawakili wa Leviston wamedai kuwa wasilisho la 50 ni njia ya
kutaka kukwepa kulipa faini hiyo. Wameomba kuongezwa kwa dola milioni 10
zingine kama ‘punitive damage’ ili kumuadhibu 50 kwa kusambaza mkanda
huo.
Hatua hiyo imekuja kama surprise kwakuwa ni miezi miwili tu iliyopita
Forbes walidai kuwa rapper huyo ana utajiri wa dola milioni 155.
Jaji wa masuala ya kufilisika anatarajiwa kutoa maamuzi Alhamis hii kama
wasilisho la 50 linaweza kuchelewesha kesi hiyo. Hata hivyo rapper huyo
anaonekana kutokuwa na stress zozote na kesi hiyo.
Ijumaa iliyopita aliangusha party ya nguvu ya birthday yake huko Las
Vegas. Jumapili alitweet, “I can’t remember a year that I had this much
fun. Just good energy every were I go.”
Kupitia Instagram, rapper huyo amepost picha hiyo chini na kuandika, “Times are hard out here, LMAO.”
0 comments:
Post a Comment