Msanii wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Shamsa Ford amesema amekoma kutoka kimapenzi na watu maarufu.
Muigizaji huyo ambaye miezi michache
iliyopita alikiri kutoka kimapenzi
na rapa Nay wa Mitego, ameiambia Bongo5 kuwa sasa hivi amepata mpenzi
mpya ambaye atamweka wazi siku ya harusi yake.
“Mimi ni
mwanamke mzuri nakosaje mwanaume? Nimetimia kila idara, nina mchumba
ambaye tunapendana Mungu akijalia kiukweli natamani awe mume wangu,”
amesema.
“Nimeshatangaza
kabisa mastaa sitaki nimekoma, nimekoma kutoka kimapenzi na mastaa au
kumtangaza mpenzi wangu kwenye mitandao. Mpenzi wangu watamjua siku ya
harusi yangu. Unajua mastaa wana mambo mengi sana na kuendelea nao ni
kupoteza muda tu” amesisitiza Shamsa Ford.
Hata hivyo Shamsa hakutaka kuzungumzia sababu ya kuachana na Nay.
0 comments:
Post a Comment