Akihojiwa na DW amesema ni kweli sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ni
mbovu na inapelekwa bungeni kuibadilisha. Alipoulizwa kwamba kama
amekiri sheria hiyo ni mbovu ikiwa itafutwa na maamzi ya kulifungia
Mawio yatabatilishwa kwa vile yalifanyika kwa kutumia sheria mbovu?
Akasema sheria hata kama ni mbovu lazima iheshimike hivyo maamzi
yatabaki pale pale.
Kuhusu bunge kurushwa live Nape amesema watumishi wa serikali walikuwa
wakiiba muda wa kazi kutazama bunge. Alipoulizwa kwa nini hatua za
kiutendaji zisichukuliwe badala ya kusitisha matangazo na kwa nini
mwanzoni alisingizia gharama. Akajibu kwamba suala hilo si la serikali
bali bunge "Kwanza hili suala si la serikali, bunge liliona ni kuna
redio 125 nchi hii na wote hawawezi kuleta mitambo yao hapa hivyo
wakatengeneza studio ambayo redio zote zinaweza kupata matangazo"
alisema.
Alipobanwa kwamba kwa nini redio na Tv zilizo na uwezo wa kurusha moja
kwa moja zilizuiliwa? Akajibu, mbona South Africa wanafanya hivyo na
hakuna malalamiko? "Nchi nyingine kama South Africa inaonyesha masaa 8
live na baada ya hapo wanarekodi huko mbona hawalalamik

0 comments:
Post a Comment