
Kesi inayomkabili Isaac Abakuk ambaye alishitakiwa kumtukana Rais John Magufulikwenye ukurasa wake wa facebook imesikilizwa leo June 08 2016 kwenye Mahakama Kuu kanda ya Arusha ambapo maamuzi yametolewa ambapo mshitakiwa ametakiwa kulipa millioni 7 au kutumikia kifungo cha miaka 3 gerezani.
Mshtakiwa amekiri kutenda kosa hilo ambapo mahakama imeamuru alipe fedha hizo kwa awamu mbili, katika awamu ya kwanza atalipa July 8 2016 sh mil 3.5 na August 8 2016 atalipa kiasi kilichobaki cha sh mil 3.5.
#UpdateTWO Mahakama imeamuru alipe kwa awamu mbili, July8 milioni 3.5 alafu August 8 amalizie milioni 3.5. #Arusha


0 comments:
Post a Comment