Mtayarishaji wa muziki mkongwe na mmiliki wa Studio ya Mj Records,
Master Jay amefunguka na kusema kuwa yeye aliwahi kuoa mapema kutokana
na ‘presha’ (shinikizo) la wazazi wake na jamii kiujumla.
Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na EATV, Master Jay
amesema aliweza kumuoa mke wake wa kwanza akiwa mdogo kutokana na wazazi
wake na kudai kuwa licha ya wao kuachana lakini mzazi mwenzake huyo ni
bonge la mwanamke kwani anatabia njema na roho ya upendo sema ilifika
mahali moyo wake uligoma tu lakini hakuwa na ubaya wowote ule.
Unajua wazazi wanakuwa wameshakupeleka shule baada ya hapo nilipomaliza,
nikaanzisha biashara, ndiyo hapo wakaanza ohh miaka inaenda sijui nini
na nini, yaani kuna vitu vingine tunapewa presha fulani hivi hivyo
unajikuta unalazimisha vitu ili viwe vile ambavyo wao wanataka, hivyo
hata mimi ilikuwa ni presha. Lakini sijutii kwani kutokana na ndoa yangu
hiyo ya kwanza walitoka watoto wangu watatu ambao nawapenda sana,”
alisema Master Jay.
Mbali na hilo Master Jay ameeleza kuwa hakulazimishwa kumuoa mwanamke
huyo wala hakuletewa bali alimpenda mwenyewe na yeye ndiye aliyempeleka
nyumbani kwao na kudai kuwa mpaka leo yule mwanamke ni bonge la mtu
sababu anajiheshimu sana na anasifa zote sema ni vile moyo wake
ulipishana naye.

0 comments:
Post a Comment