Friday, 26 February 2016

Wateja wa NMB kujishindia fedha

BENKI ya NMB imezindua promosheni mpya kwa ajili ya wateja wake ya kuweza kujishindia fedha taslimu.
Promosheni hiyo itakayojulikana kama ‘Pata Patia na
NMB’ itadumu kwa miezi sita, ina lengo la kuhamasisha wateja kujiwekea akiba katika akaunti zao na kuweza kujishindia fedha.
Kaimu Mkuu Kitengo cha wateja binafsi, Boma Raballa alisema “NMB imeanzisha promosheni hii kwa lengo maalumu la kuhamasisha wateja wake kujiwekea akiba katika akaunti zao”.
Alisema pia wateja wapya kujiunga na NMB kwa kufungua akaunti na kuweka akiba huku wakiwa na nafasi kubwa ya kujishindia fedha.
Raballa alisema mteja anatakiwa kuweka kiasi kisichopungua Sh 50,000 na kuweza kujishindia kuanzia Sh 100,000 hadi Sh milioni tatu papo hapo.
“Tunatarajia kuwafikia washindi 144 kwa miezi sita na tukimpata mshindi atapigiwa simu na ataelekezwa namna ya kushiriki promosheni hiyo,” alisema.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa NMB, Rahma Mwapachu alisema “Tayari tumepata kibali kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha na tuna imani shindano hili litawanufaisha wengi na kufikia malengo yao waliyojiwekea”.

0 comments:

Post a Comment