MUIGIZAJI mkongwe nchini, Salome Nonge ‘Mama Abdul’ amewacharukia mastaa
wa filamu Bongo kwa kususia kujitokeza katika uzinduzi wa
kitabu cha
Kanumba.
Mama Abdul aliyasema hayo muda mfupi baada ya kuisha kwa uzinduzi wa
kitabu hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa
Landmark, Ubungo Riverside ambapo alisikitishwa kutokana na marehemu
kuwa mchango mkubwa katika tasnia ya filamu.
“Wasanii wetu ni wanafiki, wanapata wapi jeuri ya kumtenga Mama Kanumba
wakati kwenye msiba walikuwa wote? Au tuseme wameona kwenye uzinduzi
hakuna namna ya kupiga dili kama walivyozoea watawakosa watu wa kuwauzia
sura.”
“Wamenikera, halafu wakimuona Mama Kanumba wanajifanya kumsalimia
kinafiki. Bongo hakuna kama Kanumba waache kujishauwa,” alisema Mama
Abdul.
0 comments:
Post a Comment