Inadaiwa Lissu alitoa maneno ya uchochezi nje ya mahakama ya Kisutu kwa kumuita Rais ‘dikteta uchwara’, mtuhumiwa amedhaminiwa na wadhamini wawili na kesi imeahirishwa mpaka August 02 mwaka huu itakapoanza kusikilizwa. Nje ya mahakama ya Kisutu, Lissu ameyazungumza haya……….
’Mimi nilidhani kwamba baada ya kauli yangu wenye busara wangenyamaza kimya lakini inaelekea busara inaonekana ni bidhaa adimu wameyaleta mahakamani, mimi na jopo langu la mawakili tutapata fursa ya kumuita huyo niliyemuita dikteta ‘uchwara’ kuja mahakamani kuiambia mahakama kuwa yeye si dikteta uchwara‘

0 comments:
Post a Comment