Jana wafuasi wa UKAWA walitiwa mbaroni baada ya kutoke mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kumkashifu
Mtukufu Mkuu sana, Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli.
Baadhi ya Mabango yalikuwa yanasomeka...
Dikteta uchwara utashindwa
Dikteta uchwara nenda Burundi
Maoni Yangu;
Kuna msemo usemao Delegatus Non Potest Delegare wakimaanisha la
kujitakia halina majuto. Hawa wafuasi naona wamejitakia au wametumwa na
viongozi wao uchwara kubeba mabango ya kashfa kwa Rais. Mbowe alikuwepo
mahakamani, kwanini yeye hakubeba bango la kashfa? Kwanini awatumie
wafuasi wachache wasiojielewa?
Hivi nalo hili mtalalamika kuonewa?
Kwanini hamuheshimu Taasisi ya Urais?
Kwanini hamuheshimu Rais?
Mnataka nini hasa wana wa upinzani?

0 comments:
Post a Comment