Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii
kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana
na hatia ya kumtukana Rais na kuhukumiwa faini ya Sh7 milioni au
kifungo.
Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya kumtukana
Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa kulipa fedha
hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela
miaka mitatu.
Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (Chadema), Ephata Nanyaro
ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa
wameshakusanya Sh 800,000/- ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa
simu.
Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote.
"Tumesikia familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi
tumejitolea kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi
julai,” alisema.

0 comments:
Post a Comment