MKUTANO
wa tatu wa Bunge la 11 unaendelea tena leo mjini Dodoma, na wiki hii,
Serikali itawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha
wa 2016/17 ya wizara tatu, ikiwemo bajeti ya Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Ratiba
mpya iliyotolewa wiki iliyopita inaonesha wizara nyingine
zitakazowasilisha bajeti zao wiki hii ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto itakayojadiliwa kwa siku mbili.
Mwaka
jana, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (wakati huo Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo) ilitengewa jumla ya Sh bilioni
29.4 kati ya hizo Sh bilioni tano zilikuwa ni fedha za maendeleo na Sh
bilioni 24.4 za matumizi ya kawaida.
Kwa
upande wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, bajeti iliyopita,
ilitengewa Sh bilioni 1.7 kwa ajili ya Matumizi ya kawaida na matumizi
ya maendeleo ili iweze kutekeleza majukumu yake katika mwaka 2015/16.
Kati
ya fedha hizo Sh bilioni 1.4 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Sh
milioni 239.1 ni kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo. Kwa upande wa
Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo kwa
muda mrefu , bajeti imekuwa ikilalamikiwa kuwa ndogo, imejumuisha wizara
mbili ya Afya pamoja na ile ya Jinsia, Jamii na Watoto.

0 comments:
Post a Comment