Wakati baadhi ya vyama vya siasa vimetangaza kujitoa uchaguzi wa marudio
Zanzibar, tume ya uchaguzi -ZEC- imetoa msimamao wake na kusema
wagombea wote ni halali na watagombea nafasi
zao kwa vile hakuna hata
chama kimoja kilichofuata sheria na kanuni za uchaguzi.
Msimaamo huo wa tume umetolewa na mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi ya
Zanzibar Jecha Salum Jecha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari
ambapo amesema kuna utaratibu wakujitoa na kwa mujibu wa sheria na
kanuni za uchaguzi hakuna chama kilichofuata kanuni ikiwa ni pamoja na
wadhamini wawagombea kutangaza kuondoa udhamini wao, hivyo wagombea wote
wa urais, uwakilshi na udiwani wote bado ni halali.
Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi vyama amabvyo vimethibitisha kushiriki ni
pamoja na CCM, TADEA, ADC, CCK, AFP, SAU, TLP, huku CUF, NRA, CHAUMA,
DP, Jahazi asilia na ACT Wazalendo ambao mgombea wake Khamis Lilla
ametangaza kugombea huku chama chake kikimufukuza uanachama.
0 comments:
Post a Comment