KUNDI la wapiganaji la ISIS limemuua kwa kumkata kichwa kijana mmoja
baada ya kumkuta akisikiliza muziki wa Pop unaoimbwa na wasanii wa
Marekani akiwa kwenye baa ya baba yake.
Kijana huyo, Ayham Hussein (15) alikamatwa mjini Mosul, Iraq baada ya
wapiganaji waliokuwa
kwenye doria kumsikia akisikiliza muziki huo.
Mauaji hayo yalifanyika nje ya msikiti baada ya Hussein kutiwa hatiani
na mwili wake umekabidhiwa kwa wazazi wake kwa taratibu za mazishi.
Mbali na kuuawa Hussein, vijana wengine wawili nao wameuawa kwa kupigwa risasi nje ya msikiti kwa kutohudhuria Swala ya Ijumaa.
ISIS walipiga marufuku miziki ya nchi za magharibi kupigwa kwenye maeneo
yao huku sababu kuu ikitajwa kuwa miziki hiyo ni chanzo cha vitendo
viovu, majaribu pamoja na kumfanya mtu kushindwa kujifunza Koran hivyo
kumsahau Mungu.
0 comments:
Post a Comment