Jumamosi ya February 20 ulipigwa mchezo
wenye upinzani na historia kubwa katika nchi hii, hiyo ndio siku ambayo
ulipigwa mchezo wa Simba na
Yanga, huu ulikuwa mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania bara, mchezo ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Simba. Lakini kuna baadhi ya mashabiki wa Simba wanasema refa aliipendelea Yanga na kumuonesha kadi nyekundu Abdi Banda.
Afisa habari wa Yanga Jerry Muro ana majibu haya kwa wale wanaosema Yanga ilipendelewa >>> “Baadhi
ya mashabiki tumewasikia kwenye vyombo vya habari wakilalamika Yanga
ilipendelewa, lakini niwaambie kocha wao ambae ni mtaalam Jackson Mayanja
amehojiwa leo lakini hakusema refa alipendelea na kueleza kuwa kafungwa
kwa sababu hesabu zake zilikataa, sasa wao na kocha nani mtaalam?”
0 comments:
Post a Comment