Monday, 9 May 2016

VIDEO: Tukio lililomfanya Malimi Busungu wa Yanga kuwa nje ya uwanja mwezi mzima

May 7 2016 mchezaji wa Yanga ambaye pia amewahi kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Malimi Busungu aliingia kwenye headlines baada ya kugongana na kipa wa GD Esperanca ya Angola ,Yuri JKose Tavazes dakika ya 53,Busungu alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa nje ya uwanja na baadae kuwahishwa hospitali.
Leo May 9 2016 rasmi uongozi wa Yanga kupitia kwa afisa habari wake Jerry Murowamethibitisha kuwa mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja mwezi, kwa maana hatamalizia mechi za msimu zilizosalia “Ni kweli Busungu ameumia  katika mbavu na atakuwa nje ya uwanja mwezi”


0 comments:

Post a Comment