Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko
5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali
mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa
TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.
Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi
ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea
nchini Brazil kupitia Zanzibar.
Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Milioni 246.
Sukari hiyo imegawiwa kwa taasisi 31 mkoani humo baada ya TFDA kuthibitisha kuwa sukari iko salama kwa matumizi ya binadamu.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo Mkurugenzi wa huduma na
Elimu kwa mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema baada ya kukamatwa kwa
bidhaa hizo TRA kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali ikiwemo
ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, iliamriwa sukari hiyo kuigawa kwa watu
wenye uhitaji katika mkoa huo zikiwemo taasisi za elimu, Afya, kambi za
wazee na Jeshi la magereza.
Chanzo: TBC
0 comments:
Post a Comment