Monday, 9 May 2016

CONFIRMED: Huyu ndio staa wa Simba aliyesaini Yanga


Baada ya headlines za muda mrefu kuhusishwa kutaka kuhama klabu ya Simba na kuhitajika na watani wa jadi wa Simba klabu ya Dar es Salaam Young Africans, hatimae leo May 9 2016 ushahidi wa picha umewekwa wazi baada ya beki Hassan Kessy kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga.
3f64ae89-afd6-43dd-a3b8-5a28badce2db
Kuanzia kushoto ni Kaimu katibu mkuu wa Yanga BarakaHassan Kessy na meneja wa mchezaji huyo Athumani Tippo
Kessy ambaye awali aliripotiwa kuwa na mgogoro na klabu ya Simba hususani baada ya kumchezea faulo mchezaji wa Toto Africans Edward Christopher alionyeshwa kadi nyekundu na siku tatu baadae Simba wakatangaza kumfungia mechi tano kutokana na kosa hilo lakini mkataba wake Simba ulikuwa unaisha.

0 comments:

Post a Comment