Thursday, 26 May 2016

AUDIO: Alichosema Ole-Sendeka kwenye mazishi ya Kabwe na kuhusu kusimamishwa kwake kazi


Christopher Ole-Sendeka ambaye ni msemaji mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) alikua miongoni mwa waliohudhuria mazishi ya Wilson Kabwe aliyekua mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam aliyefariki siku chache baada ya kusimamishwa kazi na Rais Magufuli ili kupisha uchunguzi kwa tuhuma zilizomkabili.
Kwenye maziko ya Marehemu Kabwe yaliyofanyika kata ya Mamba Mpinji wilayani Same Kilimanjaro viongozi mbalimbali wa serikali walihudhuria akiwemo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick, kulikua na Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam pia Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene aliyemuwakilisha Rais Magufuli.
Ole Sendeka, Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Said Meck na Waziri Simbachawene.
Ole Sendeka wa kwanza kushoto mwenye miwani, Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Said Meck na Waziri Simbachawene.
Msemaji mkuu wa CCM Ole-Sendeka alisema yafuatayo >>> ‘Alifanya mambo mengi mazuri, kutuhumiwa ni jambo moja na kupatikana na hatia ni jambo tofauti, yeye alituhumiwa na hakupatikana na hatia mpaka sasa tunapomsindikiza, tuna kila sababu ya kusema Kabwe ni mtumishi muaminifu, muadilifu maana anamaliza safari yake akiwa hajapatikana na hatia
Unaweza kumsikiliza zaidi Ole-Sendeka kwa kubonyeza play hapa chini


0 comments:

Post a Comment