Na EleuteriMangi-MAELEZO.
Waziri wa NchiOfisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene amewaagiza wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuhakikisha wanampatia taarifa ifikapo Aprili 3, 2016 ni lini mradi huo utaanza kutoa huduma.
Uamuzi huo wa Waziri Simbachawene unafuatia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa kikao na wadau hao Machi 31, 2016 kilichofanyika ofisi za DART jijini Dar es salaam ili kuhakikisha wanatoa huduma ya usafiri wa uhakika kwa Watanzania na hasa wakazi wa jiji hilo.“Kama mambo yote yataenda vizuri mradi huu utaanza mapema angalau mabasi 50 yaanze kutoa huduma mapema iwezekanavyo” alisema Simbachawene.
Simbachawene alisema kuwa hadi sasa mabasi mawili yamesha anza kufanya majaribio katika barabara za mradi huo na kuwahimiza wadau hao waongeze idadi ya mabasi yanayofanya majaribio angalau yafike 15 ili madereva wazoee barabara kabla ya mradi kuanza kutoa huduma rasmi.
Ili kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo, Simachawene amewataka wadau hao wa mradi wa mabasi yaendayo haraka wawe na utaratibu wa kukutana kila siku kwa kuzingatia kazi walizojipangia na kuangalia utekelezaji wake umefikia wapi na kumpatia taarifa kila baada ya siku mbili.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Kaimu Mtendaji Mkuu Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Lwekatare akitoa taarifa ya mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Katikati ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jaffo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene (wa pili kulia) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
0 comments:
Post a Comment