Thursday, 21 April 2016

Makonda aanza kupambana na wafanyakazi hewa jijini Dar..Tazama Video hapa


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta watumishi hewa katika Manispaa za jiji la Dar es Salaam bado inaendelea baada kubaini njia chafu wanazotumia watumishi hewa hao.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar, Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kioo kwa nchi hivyo jitihada zinaendelea ya kufanikisha zoezi hilo na  kazi hiyo itafanywa sekta kwa sekta.

Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya katika jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi nyingine yeyote mpaka wamalize kuwatafuta watumishi hewa kwa kutumia malipo ya watumishi 
(Pay Roll) kutoka kwenye taasisi za fedha.

Makonda amesema idadi ya watumishi hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre Simbachawene ni ndogo katika jiji la Dar es Salaam hivyo kazi lazima iwe endelevu.

Amesema kuwa watumishi hewa hawawezi wakawa wanalipwa mshahara huku wanaofanya kazi kwa moyo mmoja wanajisikia vibaya hivyo ni lazima watafutwe na wachukuliwe hatua na vyombo vya dola.

Mkuu Mkoa amesema kuwa kati ya watumishi hewa 71 ni watumishi 34 hewa wamefunguliwa mashitaka katika mahakama mbalimbali kutokana kuchukua fedha wasioifanyia kazi.

0 comments:

Post a Comment