Chris Brown amesema alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna kabla ya tuzo za Grammy mwaka 2009.
Katika kipande kifupi cha makala yake ya ‘Karibu katika maisha
yangu’,mwanamuziki huyo wa mtindo wa R & B amesema uhusiano wao
ulikuwa kama ndoto lakini akajihisi kama hayawani.
“Nilikuwa katika kilele cha dunia,nyimbo zangu zikiongoza,nikapendwa na
wengi nchini Marekani kabla ya kuanguka hadi kuwa adui wa umma,” alisema
Chris Brown.
Kesi yake ilisitishwa mwaka jana baada ya jaji mmoja kusema kuwa nyota
huyo amekamilisha mahitaji yake yote na kufunga kesi hiyo rasmi.
Pia kwenye makala hiyo inayowaonyesha Jennifer Lopez,Usher,Mike
Tyson,Jamie Fox na Rita Ora, Chris Brown anasema, “Nilihisi kama nyota,
lakini nilijiharibia. Nilikuwa nikilala.Sikuweza kula,nilijihisi
maarufu,” alikiri.
Source: BBC

0 comments:
Post a Comment