Monday, 14 March 2016

Ndalichako: Mikopo ya HESLB ilipwe

     Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako
SERIKALI imeendelea kuwasisitiza Watanzania walionufaika kwa mikopo ya elimu ya juu kurejesha fedha walizokopa ili wengine wanufaishwe nayo pia. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisisitiza hivyo hivi karibuni, alipokuwa akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St Joseph cha Dar es Salaam waliogoma kuingia darasani kwa sababu mbalimbali.
Ndalichako alisema, wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini wanaohamasishana kugoma hata wakifukuzwa vyuoni ni lazima warejeshe fedha za Serikali walizokopa. “Wanafunzi mnapofanya migomo mtambue kuwa kuna fedha za Serikali mmechukua na mwisho wa siku ikitokea kutokuelewana mtafukuzwa na kulazimika kuzilipa,” alisema.
Alisema, Watanzania wote ambao ni wanufaika wa mikopo iliyotolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), warejeshe fedha hizo na ikiwezekana kwa mkupuo. Kwa mujibu wa waziri huyo, wapo wanafunzi walisoma vizuri kupitia mikopo hiyo na sasa wana kazi na vipato vizuri, lakini hawajarejesha fedha hizo.
Aliwataka muaanze sasa kuzirejesha. Alisema, wanufaika wote wanaodaiwa wameorodheshwa hivyo, watakapopelekewa barua walipe madeni yao. Alisema hiyo ni kwa makundi yote ya wanufaika. M

0 comments:

Post a Comment