Wednesday, 11 July 2018

BREAKING: Ambulance imekamatwa na Kilo 800 za Mirungi


Leo July 11, 2018 Gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) ya Hospitali ya Wilaya ya Tarime yenye namba za DFPA 2955 imekamatwa ikiwa imebeba Kilo 800 za Dawa za Kulevya aina ya Mirungi.
RPC wa Mara Juma Ndaki amethibitisha kukamatwa kwa gari hilo na watu wawili, gari ilikuwa inatoka Mwanza kwenda Tarime.
Kamanda Ndaki amesema “Tumewakamata na Mirungi Kilo 800, tunawashikilia watu wawili, gari ilikuwa inatoka Mwanza kwenda Tarime, ushauri wangu tuwe makini tunapoajiri Madereva serikalini,”
RPC mpya Mbeya alivyofanya operesheni stendi ya Mabasi Alfajiri

Thursday, 19 October 2017

Jeshi la Polisi Dar es salaam linazungumza

AyoTV ipo na wewe wakati wote kukuletea matukio ya moja kwa moja (LIVE) na sasa AyoTV ipo live kutoka kwenye makao ya Polisi Dar es salaam… bonyeza play hapa chini kutazama live kila kinachosemwa
ULIPITWA? Tundu Lissu katolewa ICU, aliona jua kwa mara ya kwanza toka apigwe risasi… bonyeza play hapa chini kufahamu kila kitu


Tuesday, 3 October 2017

Wednesday, 19 April 2017

VIDEO: Maswali matatu ya Mbunge Professor J Bungeni leo

Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu Professor J, April 19, 2017  alisimama Bungeni kuuliza maswali kwa serikali ikiwemo changamoto ya maji iliyopo jimboni kwake na majibu yakatolewa na Naibu Waziri wa maji na umwagiliaji Isack Kamwelwe

VIDEO: ‘Serikali inafanya jitihada lakini haina majibu sahihi’ –Jumaa Aweso


Thursday, 2 February 2017

Ridhiwani Kikwete Afafanua Kwanini ilikuwa ni Aibu Kwa TFF na Waziri, Diamond Kukabidhiwa Bendera Kwenda Gabon


Ridhiwani Kikwete aliingia kwenye headlines mwanzoni mwa mwezi uliopita pale alipoandika post Instagram akisikitishwa na kitendo cha Diamond kukabidhiwa bendera na Waziri wa michezo, Nape Nnauye kwenda kutumbuiza kwenye ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika, nchini Gabon.



Mbunge huyo wa Chalinze, amedai kuwa, post yake haikumlenga Diamond, bali aliwapa ujumbe shirikisho la soka Tanzania, TFF na Waziri Nape.


“Kilichonifanya niandike ile meseji ni baada ya kuona kwamba mashindano yanayoenda kufanyika ni ya mpira wa miguu, sisi tunayo timu ya taifa ya mpira wa miguu, lakini to our surprise, badala ya kutoa bendera kwa timu ya mpira wa miguu, tunawapa waburudishaji kwa maana ya wanamuziki kama Diamond,”
Ridhiwani alisema kwenye mahojiano na The Beauty TV.

“Matarajio yetu sisi ni kumuona kapteni wa taifa ndiye anayepokea bendera na sio wanamuziki,” ameongeza. “Pia watu wa TFF, kwamba nao wanashangilia yale anayoyafanya waziri?” Hivi vitu lazima tuwe serious.”

“Diamond yeye nampongeza sana, kwa hatua aliyofika, anafanya kazi nzuri, na ndio maana watu wamemuona, wamempa nafasi ya kwenda kutumbuiza ambayo sisi kama watanzania we feel proud. Lakini the bottom line ni kwamba, nini agenda kubwa inayomfanya Diamond aende Gabon? Ni mpira wa miguu, Diamond si mchezaji wa mpira wa miguu, hata kama labda anashabikia mpira wa miguu, lakini yeye ni mshabiki tu, wanaoenda kushiriki pale ni wachezaji.”

Ridhiwani amekiri kuwa kitendo hicho kilimsikitisha na ndio maana hakupenda kukaa kimya.

“Si kwamba sikupenda kwasababu amepewa Diamond, hapana, sikupenda kwa sababu, matarajio ya mimi mpenzi wa mpira ni kumuona kapteni wangu wa timu ya taifa anapokea bendera kwa niaba ya watanzania wote, anakwenda kutuwakilisha kule, hata kama tutashindwa, hata kama tutafanikiwa lakini anayetakiwa kwenda kule ni kapteni wa timu ya mpira wa miguu kwenda kutuwakilisha kama taifa na si vingine.”

Tuesday, 31 January 2017

Breaking News..Necta Watangaa Matokeo ya Kidato cha Nne Mwaka 2016,Tazama Matokeo Hapa..!!!


 Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne (CSEE) na QT kwa mwaka 2016. Jumla ya watahiniwa 277,283 ambao ni sawa na asilimia 70.09 ya watahiniwa waliofanya mitihani kidato cha nne 2016 wamefaulu.

Wasichana waliofaulu ni 135,859 ambao ni swa na asilimia 67.06 wakati wavulana waliofaulu ni 142,424 sawa na asilimia 73.36.

Kwa mwaka 2015, watahiniwa waliofaulu walikuwa 272,947 sawa na asilimia 67.53. Ukilinganisha na matokeo ya mwaka huu, ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.56. Idadi hii ni ya watainiwa wote, yaani watahiniwa wa shule na watahiniwa wa kujitegemea.

Bonyeza hapa kuweza kuona matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 –>CSEE 2016

Bonyeza hapa kuweza kuona matokeo ya QT mwaka 2016  –>(QT) 2016

Wanafunzi 10 Bora Kitaifa

  1.      Alfred Shauri (Feza Boys)
  2.     Cynthia Nehemiah Mchechu (St. Francis Girls)
  3.     Erick Mamuya (Marian Boys)
  4.     Jigna Chavda (St. Mary Goreth)
  5.     Naomi Tundui (Maria Girls)
  6.     Victoria Chang’a (St. Francis Girls)
  7.     Brian Johnson (Marian Boys)
  8.     Esther Mndeme (St. Mary’s Mazinde Juu)
  9.     Ally Hassan Koti (ALCP Kilasara)
  10.     Emmanuel M. Kajege (Marian Boys)


Wasichana 10 Bora Kitaifa

  1.     Cynthia Mchechu (St. Francis Girls)
  2.     Jigna Chavda (Mary Goreti)
  3.     Naomi Tundui (Maria Girls)
  4.     Victoria Chang’a (St. Francis Girls)
  5.     Esther Mndeme (St. Mary’s Mazinde Juu)
  6.     Christa Edward (St. Francis Girls)
  7.     Nelda John (Marian Girls)
  8.     Mariamu Shabani (Kifungilo Girls)
  9.     Beatrice Mwella (St. Mary’s Mazinde Juu)
  10.     Rachel Kisasa (Canossa)


Wavulana 10 Bora Kitaifa

  1.     Alfred Shauri (Feza Boys)
  2.     Erick Mamuya (Marian Boys)
  3.     Brian Johnson (Marian Boys)
  4.     Ally Koti (ALCP Kilasara)
  5.     Emmanuel Kajege (Marian Boys)
  6.     John Ng’hwaya (Nyegezi Seminary)
  7.     Clever Yohana (Living Stone Boys)
  8.     Desderius Rugabandana (Morning Star)
  9.     Kennedy Boniface (Feza Boys)
  10.     Assad Msangi (Feza Boys)


Shule 10 Bora Kitaifa

  1.     Feza Boys
  2.     St. Francis Girls
  3.     Kaizirege Junior
  4.     Marian Girls
  5.     Marian Boys
  6.     St. Aloysius Girls
  7.     Shamsiye Boys
  8.     Anwarite Girls
  9.     Kifungilo Girls
  10.     Thomas More Machrina


Shule 10 za Mwisho Kitaifa

  1.     Kitonga
  2.     Nyeburu
  3.     Masaki
  4.     Mbopo
  5.     Mbondole
  6.     Somangila Day
  7.     Dahani
  8.     Ruponda
  9.     Makiba
  10.     Kidete

ROTARY CLUB DAR ESALAAM

Mwenye shati jeupe ni President wa Rotary Club of Dar es Salaam, Mzizima anaitwa Rtn Dr Julius Mutabaazi Lugaziya..Tume induct members wawili na wamesimama besides na mentors wao..

1. Rtn Dr Hawa Mkwela mwenye kitenge, na mwenye suti nyeusi ni mentor wake Rtn Ambrose Ntangeki Nshala. 

2. Mwenye shati la pink ni new member Rtn Dr Joseph Mutagirwa Longino na Mentor wake ni Incoming President Rtn Eng Dennis Mwighusa. Hapo Wanasoma CV zao, then President anawaapisha na kuwavika pin km symbol ya kuwa new members..












Wednesday, 4 January 2017

WASANII Wanaosambaza Ujumbe wa Matumizi ya Mihadarati Kusakwa

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, ACP Mihayo Msikhela amedai wamejipanga kufanya msako dhidi ya wasanii wanaosambaza ujumbe wa matumizi ya mihadarati.

Akiongea na gazeti la Mtanzania, Kamishna huyo alisema hivi sasa wapo kwenye msako dhidi ya wasanii ambao wamekuwa wakisambaza ujumbe wa matumizi ya mihadarati hiyo kwa kuwa wasanii hao ambao ndio kioo cha jamii, sasa wamekuwa wa kwanza katika kusambaza ujumbe wa matumizi hayo.

“Mimi binafsi simfahamu Chid Benz kama ni mtu maarufu aliyekuwa akifahamika kwa kiasi hicho, lakini baada ya kumuona kwenye mitandao ya kijamii ndipo nikaanza kumfuatilia,” alisema Kamishna Msikhela.

Alisema endapo wakipata taarifa ya kwamba wanatumia hadharani na kuwakamata, basi watachukuliwa hatua kama wahalifu wengine.

“Hawa wasanii tunawasaka nao watuhumiwe kama wahalifu wengine na wakichukuliwa hatua itakuwa fundisho kubwa kwa vijana ambao walikuwa na nia ya kujiingiza katika mtandao huo,’’ alisema.

Alisema ni vema kwa vijana wasiwafuate watu maarufu ambao kwa namna moja ama nyingine wanaushawishi mkubwa kiasi katika matumizi ya dawa hizo.

Kamishna Msikhela alisema wimbi kubwa la vijana wenye umri kati ya miaka 15 na 30 ndilo ambalo linajiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya jambo ambalo ni hatari kwa Taifa.

“Vijana hawa ndio ambao wangekuwa tegemeo, vijana wa umri huo ndio ambao wangekuja kuwa viongozi wa baadaye, yaani kwa umri huo ndiyo wanaandaliwa kuwa madereva, mawaziri, wakulima, lakini leo wanakuwa mateja, ni jambo la hatari sana,’’ alisema.

Kamishna Msikhela alisema Jeshi la Polisi kwa sasa liko katika mkakati maalumu wa kuhakikisha elimu katika jamii inatolewa ili wananchi waweze kuelimika.

Alisema ulimaji wa bangi mashambani ni mkubwa kuliko mirungi, lakini aliongeza kuwa kama mateja mitaani wanapungua basi hata uingizaji wa dawa hizo kwa sasa nao umepungua.

FEROOZ " Inaniwia Vigumu Kuacha Madawa ya Kulevya"

Msanii mkongwe wa muziki Ferooz Mrisho ambaye katika miaka ya 2000 alitamba na wimbo wa Starehe ambaye kwa sasa ameathirika na dawa na matumizi ya Madawa ya kulevya, amedai inamuwia vigumu kuachana na matumizi ya dawa hizo. Muimbaji huyo amedai amejikuta akitenga bajeti kubwa ya fedha kwa matumizi ya kutumia dawa.

“Ninawaomba wasanii wenzangu wasitumie dawa maana ni vigumu kuacha. Natamani sana kurudi kama zamani ili heshima yangu iwepo ila inanisumbua, lakini naamini iko siku,” Ferooz aliliambia gazeti la Mtanzania. Hata hivyo muimbaji huyo alipoulizwa ni wapi anaponunua Madawa hayo hakuwa tayari kutaja.

Siku 16 kabla ya kuapishwa, haya ni maoni mapya ya Wamarekani kuhusu Donald Trump


Zikiwa zimebaki siku 16 kabla ya kuapishwa na kuingia IKULU ya White House kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump, imetoka ripoti ya utafiti wa maoni ya watu nchini humo uliofanywa na Kampuni ya Gallup umeonesha kuwa, ni 46% tu ya watu ambao wanaamini kuwa Donald Trump anaweza kutatua misukosuko ya kimataifa.
Utafiti huu umeonesha kuwa, zaidi ya 50% ya wamarekani wana mashaka juu ya uwezo wa Rais mteule Donald Trump katika kutatua migogoro ya kimataifa, kutumia nguvu ya kijeshi kwa busara, au kuepuka kashfa kubwa katika utawala wake, akilinganishwa na Marais waliopita.
Takwimu zinaonesha asilimia 70 ya wamarekani walikuwa na imani na Barack Obama, George W Bush na Bill Clinton katika maeneo hayo kabla yao kuingia madarakani.
Utafiti huo pia umeonesha maoni ya Wamarekani kama ifuatavyo.
47% Wanaamini kuwa Trump atatumia kwa busara nguvu za kijeshi
44% Wanaona anaweza kuzuia kashfa kubwa kutokea kwenye serikali yake.
60% Wameeleza imani yao kwa Trump katika kushirikiana kwa ufanisi na bunge.
59% Wanaamini atashughulikia vizuri uchumi.
55% Wanaona ataweza kulinda maslahi ya Marekani nje ya nchi akiwa Rais.
53% Wanaamini ataweza kusimamia ofisi ya ikulu ya Marekani asilimia.
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump anatarajia kuapishwa rasmi na kuchukua madaraka ya Urais wa 45 wa Marekani January 20, 2017.
VIDEO: Wapo Watanzania wanaoishi Marekani na hawaamini kama Donald Trump atatekeleza kauli yake ya kuwaondoa wahamiaji wote nchini humo. Mtazame Mtanzania huyu anayeishi Marekani.

TANZIA: Anna Senkoro, mwanamke wa kwanza kugombea Urais nchini Tanzania(2005), afariki dunia

Aliyekuwa mgombea urais wa kike wa kwanza Tanzania (Uchaguzi 2005) kupitia chama cha APPT-Maendeleo, Dr. Anna Claudia Senkoro ameaga dunia.

Inadaiwa aliugua ghafla usiku wa kuamkia leo na amefariki baada ya kukimbizwa hospitali asubuhi ya leo.

Msiba upo nyumbani kwake, Tabata Segerea jijini Dar.

Taarifa zaidi zitafuatia...

IDRIS Sultan – Nando is on the recovery road


It is certainly going to be rough year for Nando, especially now that few of his friends are penning out words of encouragement on social media. Apart from Feza Kessy and Nikki Mbishi who are crying out to fans support, former Big Brother Africa winner, Idris Sultan and had to say to Bongo5.


“I did not see the need to post anything about Nando firstly because he is not my friend. We are more of acquaintances ever since we were in big brother in 2014. We used to meet in events and parties but I still cannot consider him as close. Together with some of the housemates we have had some hard time to look for his mother’s contact and make her aware of her sons’ state therefore he is now checked into rehab at Kigamboni. I can gladly say he on the recovery road.”

“Nando is a smart, creative and real than I can be, so I can admit at first I did not know he was using drugs until he confessed to me. Honestly, I did not expect him to be in such a state however his appearance could tell a lot. Telling him to stop was not necessary since at the end of the day it’s his initiative to decide so.”

He adds, “As for now, together with my friends, his family and close friends we have taken responsibility to contribute money and make sure he gets assistance till the day they will release him. However, my main goal towards Nando is once he is released I will get mentors to regularly talk to him in that he does not slip as former stars have done. I will support him because he is an incredible person. It my prayer together with former big brother housemates that Nando will fully recover.

YOUNG Dee Azijibu Tetesi za Kurudia Unga

Hatimaye rapper Young Dee amejibu kwa ufupi kuhusiana na tetesi kuwa amerudi tena kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Akiandika maneno mafupi sana kwenye post yake mpya ya Instagram, Young Dee amedai kuwa ‘muda utaongea.’

“Time will Tell… Mi sina tatizo na mtu… Tuombeane kheri tu… Siwezi shindana na maneno,” ameandika rapper huyo.

Wiki hii tetesi za kuwa Dee amerejea tena kwenye utumiaji wa dawa hizo zilianza kufuatia maneno ya meneja wake Max mtandaoni. Max alida kuwa rapper huyo ameanza tena kuubwia unga na kwamba amechoka kusumbuka naye.

Tetesi za Young Dee zimekuja katika kipindi ambacho watanzania wanasikitishwa na hali walizonazo Chidi Benz na Nando kutokana na kuathirika vibaya na madawa hayo.

Friday, 16 December 2016

Wednesday, 14 December 2016

Wednesday, 7 December 2016

Trump Kusitisha Uagizwaji wa Ndege Mpya za Air Force One

a-deal-for-donald-trump-b
Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump amesema anataka kufuta ombi la ununuzi wa ndege mpya za Air Force One ambazo hutumiwa na marais wa Marekani.
Wiki sita kabla ya kuchaguliwa, aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa: “Boeing wanaunda ndege mpya aina ya 747 Air Force One za kutumiwa na marais siku zijazo, lakini gharama yake imezidi, zaidi ya $4 billion. Futa oda hiyo!”
boeing
Serikali ya Marekani iliingia kwenye mkataba na kampuni ya Boeing ili kutengenezwa kwa ndege hizo mbili au zaidi za kuwabeba marais.
Ndege hizo zilitarajiwa kukamilika na kuanza kutumiwa mwaka 2024.
Hisa za kampuni ya ndege ya Boeing zilishuka kwa zaidi ya 1% baada ya ujumbe huo wa Trumpp kwenye Twitter, ingawa zilijikwamua baadaye.
Trump hatarajiwi kutumia ndege hizo mpya, iwapo hatashinda uchaguzi wa muhula wa pili wa mwaka 2020.

ALICHOANDIKA Darassa Baada ya Dereva Kukamatwa Akicheza Wimbo Wake Huku Akiendesha Gari

Msanii wa Bongofleva Darassa ambaye kwa sasa anafanya vizuri na hit single ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Muziki’ ameamua kuweka wazi mtazamo wake kuhusu ile video iliyosambaa ikionesha vijana wakicheza wimbo wake  huku dereva akiacha  gari likienda.

Vijana hao wamekamatwa na polisi na Darassa ameamua kutoa mawazo yake kuhusiana na kitendo hicho ambacho kimewafanya vijana hao kukamatwa na polisi Itigi Singida, Darassa ametuamia account yake ya instagram kuandika ujumbe kuoneshwa kuguswa na

“Hawa ndugu zetu nimepata taarifa wamekamatwa kwa kosa la kutaka kusababisha ajali na unaweza kuona Kama mchezo ulielekea kubaya, ingeweza kua Tatizo kwao Au kumu sababishia mwingine, Naskia watakua mahakamani Leo I’m not so sure naendelea kufatilia”

“Nawaombea Tatizo hili Mungu awafanyie wepesi I’m sure wamejifunza Hawawezi kufanya tena mistake Kama Hii itokee, mizuka feelings mtu anaweza kufanya kitu njee ya mipango yake sometimes, Mungu awasaidie 🙏🏽 LENGO NI KUJENGA DUNIA KUA SEHEMU NZURI NA SALAMA KUISHI #Muziki“

Tuesday, 6 December 2016

Ripoti ya Hospitali Kuhusu kilichosababisha mchezaji wa Mbao FC kufia uwanjani




Baada ya kufariki uwanjani kwa mshambuliaji wa timu ya Mbao FC Ismail Khalfan siku ya Jumapili ya December 4, leo December 6 2016 imetoka ripoti ya kilichosababisha kifo cha mchezaji huyo wakati wa mchezo kati ya Mbao FC dhidi ya Mwadui FC.

Ripoti iliyotolewa na hospitali ya mkoa wa Kagera kuhusiana na kifo cha mchezaji huyo, kupitia kwa jeshi la Polisi, Ismail alifariki uwanjani kutokana na kumpata tatizo la kusimama ghafla kwa moyo (sudden Cardiac Arrest-SCA).

Kamishina Msaidizi wa Kagera, Augustin Ollomi ametoa taarifa baada ya uchunguzi wa madaktari kuhusu kifo cha mchezaji huyo ambaye hakuwa na jeraha lolote walibaini kusimama ghafla kwa moyo (sudden cardiac arrest) kulisababisha kifo

SUDDEN CARDIAC ARREST-SCA
Kwa faida yako msomaji:
Kawaida moyo una mfumo wa umeme (heart electrical system), ambao unadhibiti mapigo ya moyo, mfumo huu ukisimama basi moyo unashindwa kusukuma damu sehemu muhimu kama ubongo na ogani kuu.

Moyo ukisimama bila kurudi katika hali yake unasababisha kifo ndani ya sekunde chache na njia pekee ya msaada ni kupita electrical shock ili kushtua mfumo wa umeme wa moyo, na hii inapaswa kufanyika ndani ya sekunde chache mno.
CHANZO: salehjembe