
Leo July 11, 2018 Gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) ya Hospitali ya Wilaya ya Tarime yenye namba za DFPA 2955 imekamatwa ikiwa imebeba Kilo 800 za Dawa za Kulevya aina ya Mirungi.
RPC wa Mara Juma Ndaki amethibitisha kukamatwa kwa gari hilo na watu wawili, gari ilikuwa inatoka Mwanza kwenda Tarime.
Kamanda Ndaki amesema “Tumewakamata na Mirungi Kilo 800, tunawashikilia watu wawili, gari ilikuwa inatoka Mwanza kwenda Tarime, ushauri wangu tuwe makini tunapoajiri Madereva serikalini,”





RPC mpya Mbeya alivyofanya operesheni stendi ya Mabasi Alfajiri
0 comments:
Post a Comment