Serikali imesema kuwa nchi ina hifadhi kubwa ya chakula kutokana na
mavuno ya msimu uliopita ingawa kuna wilaya 43 zenye upungufu wa chakula
kutokana na mavuno yao kuwa chini hali iliyosababishwa na mabadiliko ya
tabia nchi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha amesema hayo
jana wakati akizindua tovuti ya wakala wa hifadhi ya chakula nchini
(NFRA) mjini Dodoma.
Mhe. Ole Nasha amesema kuwa kwa sasa serikali ipo katika hatua za mwisho
za kuratibu uuzaji wa chakula nje ya nchi bila kuathiri hifadhi ya
chakula na kuwatoa hofu wananchi wenye wasiwasi wa kukumbwa na baa la
njaa.
Naibu waziri huyo ameongeza kuwa kwa tathmini waliyoifanya imebaini kuwa
nchi nyingi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika
zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula hivyo serikali itatengeneza
mifumo mizuri ya kupeleka chakula hicho nje ya nchi.
Baada ya kuzindua tovuti hiyo ya wakala wa chakula nchini, uhifadhi wa
nyaraka za serikali kwa njia ya makaratasi umepitwa na wakati lakini pia
akaongeza kuwa hata wizara nyingine zimeanzisha tovuti lakini ni kama
zimekufa kwa sababu haziweki taarifa za mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment