
Ni September 9, 2016
ambapo Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Samia suluhu hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani tandahimba
ukitokea ikulu ndogo ya rais mtwara umepata ajali na kusababisha
majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa ligula.
Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji
cha nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya mtwara,majeruhi
walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais.
Awali kabla ya gari hilo lililobeba
wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba
waandishi wa habari liliacha njia na nusura kupinduka.
Barabara ya kutoka mtwara kuelekea
tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda
mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka
kabisa na kusababisha majeruhi.

.

.

.

0 comments:
Post a Comment