Mkali wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa mtoto wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari.
Diamond
Muimbaji huyo amesema yeye na mpenzi wake Zari wanategemea mtoto wa kiume.
“Yah kweli mimi ni baba kijacho,” Diamond alikiambia kipindi cha Leo
Tena “Natarajia Mama Tiffa anipatie tena mtoto mwingine, atakuwa wa
kiume,”
Aliongeza, “Na itakuwa mwezi Disemba mwaka huu! Baada ya hapo sitaongeza
tena mtoto mwingine, ni muda wa kula bata sasa ndio unafata na watoto
wetu wawili”
Diamond na Zari tayari wana mtoto mmoja wa kike, ‘Tiffa’ ambaye hivi karibuni atatimiza mwaka mmoja.
0 comments:
Post a Comment