Benki Zanolewa matumizi mapya kadi za ATM
WAMILIKI wa benki nchini, wamepewa mafunzo na wafanyakazi wa kampuni ya usambazaji wa Mashine ya Compulynx kuhusu namna ya uboreshaji wa ATM card,
Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Maagizo ya Benki Kuu Ya Tanzania (BoT) yanayowataka wamiliki wote wa benki kuhama katika mfumo wa ATM Card wa zamani na kuhamia katika mfumo wa ATM card za Chip.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Meneja Masoko wa Kampuni ya Compulynx, Roy Peter alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhamasisha watengenezaji wa ATM Card wa Bank kuweza kufahamu kuhusiana na huduma hyo mpya.
"Mfumo wa zamani wa kadi zilizokua zikitumika Bank hazikua na Chip Card hali iliyopelekea kua na ongezeko kubwa la wizi wa fedha katika benki.lakini katika mfumo huo mpya sio rahisi mtu kunakili data ili kufanya wizi wa miamala ya fedha." Alisema Peter.
Alisema huduma hyo inasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha upotevu wa fedha endapo mteja wa benki atatumia huduma hyo ya card zilizowekwa Chip.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Compulynx, Suhas Dalvi, alisema kampuni yake imeingia ubia na kampuni ya Entrust Datacard ambayo itasambaza vifaa vya kutengeneza ATM Card katika benki za hapa nchini.
Alisema endapo wamiliki wa benki wataelewa vyema kuhusiana na mafunzo hayo, kampuni itatoa vifaa vya kuweza kuwapa ujuzi wafanyakazi wa benki wa kitengo husika ili kutengeneza kadi hizo.
Alisema asilimia 85 ya ATM Card zote duniani zinatengenezwa na kampuni ya Entrust Datacard, hivyo inamhakikishia mteja kutumia kadi ya chip kwa kipindi cha miaka 45 bila kufanyiwa wizi wa aina yoyote.
Zaidi ya nchi 45 duniani zinatumia mfumo wa kadi za chip katika utoaji wa huduma zote ikiwa ni pamoja na hospitalini.
iko vizuri
ReplyDelete