MBUNGE
wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM) amesema aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue alikuwa ni jipu lililojificha Ikulu.
Alisema
hatua ya kutumbuliwa na Rais Dk. John Magufuli ni sahihi kwa vile
imeenzi kwa vitendo kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuwa Ikulu
ni mahali patakatifu.
Kauli
hiyo aliitoa bungeni jana, alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya
bajeti ya Wizara ya Kilimo, Migugo na Uvuvi ya mwaka 2016/17 ya Sh
bilioni 275.06.
Alisema pia kuwa hatua ya kuimarisha sekta ya kilimo huenda sambamba na uimarishaji wa maisha ya wakulima.
“Mheshimiwa
Mwenyekiti hii ni mara yangu ya kwanza kuchangia bajeti tangu
ilipoundwa Serikali ya Awamu ya Tano, kwa hali hiyo ninapenda kumpongeza
Rais Magufuli kwa kumtumbua jipu aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi (Balozi
Sefue).
Alimtaka
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba kuhakikisha
anatumbua majipu yaliyopo katika wizara yake likiwamo la wakulima hewa
kilimo kiweze kukua.
Lugola
alisema Wizara ya Kilimo ni wizara nyeti ambayo inatakiwa kuangaliwa
kwa umakini, lakini ina wakulima hewa, hivyo waziri anatakiwa
kuwatumbua.
“Jimboni kwangu vocha za pembejeo zenye thamani ya Sh milioni 46.3 zimetolewa kwa wakulima ambao hawapo.
“Kuna mmoja yupo Mwanza wamemuandika yupo kwenye jimbo langu kuwa ni mkulima wakati siyo kweli.
“Kna
mwingine na mdogo wake wapo kata nyingine wamewaandikwa kwenye vocha za
pembejeo, Nchemba tumbua jipu la wakulima hewa vinginevyo hatutapata
mali shambani,” alisema
Akizungumzia
kilimo cha pamba, alisema kuna kila sababu ya waziri huyo wa kilimo
kwenda kutumbua majipu hasa katika mbegu feki za pamba zisizoota za
Quton na ambazo zimekuwa zikisababisha kushuka kwa zao hilo mwaka hadi
mwaka.
“Hii
kampuni ya mwekezaji ni feki na wabunge wamepiga kelele kwenye bodi ya
pamba wanamkumbatia… huyo ni jipu ikiwezekana waziri ukitoka hapa nenda
ukatumbue jipu la kampuni ya Quton,” alisema Lugola
Mwigulu na bajeti bil 275.06/-
Awali
akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu
Nchema, aliomba Sh bilioni 275.06 kwa ajili ya matumizi ya kawaida
na miradi ya maendeleo.
Upinzani
Msemaji
Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi, Magdalena Sakaya, alisema kwa kipindi cha mwaka wa fedha
unaomalizika Bunge liliidhinisha Sh bilioni 60.373 kwa wizara ya mifugo
na uvuvi (sasa ni idara) zikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida na
maendeleo, kati ya hizo Sh bilioni 19. 398 zilikuwa kwa ajili ya miradi
ya maendeleo.
Alisema
taarifa ya Wizara inaonyesha hadi kufikia Machi 31, mwaka huu,
wizara ilikuwa haijapokea hata Sh moja kati ya Sh bilioni 19.4 kwa
ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
0 comments:
Post a Comment