Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo Mei 1 2016 kwa mchezo kati ya
Simba dhidi ya Azam FC kuchezwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam,
huu ni mchezo wa 26 kwa vilabu vyote na ulikuwa mchezo muhimu kwa kila
klabu hili kujiweka pazuri katika nafasi ya kuwania ubingwa.
Azam FC kabla ya mchezo dhidi ya Simba kumalizika kwa sare ya 0-0
walikuwa na point 58 wakiwa nafasi ya pili ya Ligi, wakati Simba
walikuwa nafasi ya tatu wakiwa na point 57 wakiongozwa na Yanga ambao
wapo kileleni wakiwa na point 65 na michezo 26. Sare ya mchezo huu
ilikuwa ni furaha kwa Yanga ambao wameongeza tofauti ya point kwa Azam
FC na Simba.
Kwa idadi ya mechi Simba na Azam FC huu ulikuwa ni mchezo muhimu kwao
kuhakikisha wanapata point tatu ili kuweza kupunguza tofauti yao ya
point na Yanga wanaoongoza Ligi wakiwa na tofauti ya point sita na Azam
FC anayefuatia, umuhimu wa mchezo kwa pande zote mbili ndio ulifanya
mchezo kuwa na tension kubwa kitu ambacho kilifanya wachezaji wa pande
zote kukosa magoli ya wazi wakati mwingine.
0 comments:
Post a Comment