Kama kweli Rais Magufuli atahamia katika ukaguzi wa vyeti feki akimaliza
ishu ya watumishi hewa ni wazi atapata maadui wengi na idadi yao
itakuwa kubwa kuliko anaowapata katika vita yake dhidi ya ubadhirifu.
Watumishi wenye vyeti feki katika utumishi wa umma na makampuni binafsi
ni wengi mno. Wengi wao wanafahamika na ndugu zao, marafiki zo na hata
majirani zao kwa aidha kufahamu historia zao au kwa kutumia majina
tofauti na yale waliyozaliwa nayo au kubatizwa nayo.
Wengi wa watumishi hawa wamepanda ngazi mbalimbali katika utumishi wa
umma na hata wengine kufikia ngazi za juu. Wakati mchakato wa
vitambulisho vya taifa ulipoanza suala hili linasemekana lilijitokeza
kwa kiasi kikubwa katika idara nyeti za serikali lakini kutokana na
ukubwa wake ikaamuliwa lifumbiwe macho.
Vyeti feki vinagusa karibu kada zote na katika ngazi mbalimbali mpaka hata zile ngazi zinazoonekana za watu wasioguswa.
Kama Rais JPM akiingia nakugusa huku ni wazi atakuta amegusaa idadi
kubwa ya watanzania ikiwemo ile inayomuunga mkono. Tegemezi wa vyeti
feki na vyeti feki wenyewe wataendelea kumuunga mkono zamu yao ya
kutumbuliwa ikifika? Ndio maana nachele kusema kuwa zoezi la utambuzi wa
vyeti feki litamuacha Rais Magufuli na maadui wengi kuliko atakaowapata
katika zoezi la ubadhirifu hivyo serikali yake inaweza kupoteza
umaarufu ilioanza kuupata. Homa imepanda kiasi kwamba wenye vyeti feki
wanaongoza mashambulizi makali ya ukosoaji katika mitandao ya kijamii na
popote wapatapo fursa dhidi ya utendaji wa JPM ili kumpunguza nguvu.

0 comments:
Post a Comment