Ni stori iliyoanza kuchukua headlines
April 21, 2016 Ikiwa bado tunasubiria taarifa kamili kutoka Mahakamani,
sasa Ayo TV ilimpata staa Nay wa Mitego kuthitibisha taarifa hizo za mzazi mwenza, Siwema kufungwa miaka miwili Jela.
Akizungumza staa huyo na ripota wa Ayo TV alisema…>>>’Taarifa
nimezipokea ni kweli Mzazi mwenzangu amefungwa na ninakumbuka
nilipoamka tu nikakutana na missed calls za ndugu zake kadhaa ambao
wananifahamu nikahisi kuna kitu maana sio kawaida watu kunipigia mara
kwa mara, kumpigia akaniambia Siwema amehukumiwa miaka miwili Jela
sikuamini ikanibidi nimpigie tena ndugu wa karibu naye akanithitibishia
hivyo‘ – Nay wa Mitego
‘Kosa unajua mimi nilishasahau
kwamba kitu chochote kichotokea kipindi cha nyuma kwasababu ni muda
kidogo na pia sikuwa naye kwenye mawasiliano ila niliachoambiwa kuwa
amehukumiwa miaka miwili kutoka na kosa lake, nimejikuta nimekuwa
mnyonge nimeingia imani kusikia habari hiyo’ – Nay wa Mitego
Unaweza ukabonyeza play kutazama interview ya Nay wa Mitego akizungumza kuhusu kufungwa kwa Mzazi mwenza miaka miwili Jela
0 comments:
Post a Comment