April 19
2016 Bunge la 11 lilianza rasmi bungeni Dodoma, Baadhi ya Wizara
zilianza kwa kuwasilisha bajeti zake na kutoa nafasi kwa washiriki
kuzikubali au kuzikataa. Lakini moja ya tukio lililoonekana kuwa kikwazo
kwa wengi na hata kulalamikiwa katika baadhi ya vyombo vya habari, ni
hii ya kuzuiwa kwa Waandishi wa habari kurekodi baadhi ya matukio ndani
ya bunge wakati vikao hivyo vikiendelea isipokuwa TBC pekee.
Hapa nakukutanisha na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara akizungumza kwenye Exclussive Interview na AYO TV ambapo anasema>>> ‘Kabla
ya kuja bungeni tuliona taarifa ya kuwa TBC haitaonyesha vipindi vyote,
bali itaonyesha kipindi cha maswali na majibu na vipindi vyenyewe
vitarekodiwa na vyombo vingine vyote havitatakiwa kuingia na camera‘ ;-Mwita Waitara
‘Vyombo
binafsi vinaweza kutoa taarifa kwa gharama zao, hawajaomba kulipwa na
Bunge, kitendo kilichofanyika kuwazuia waandishi ni kitendo kibaya, huu
ni uoga wa Serikali na nikuwaondoa watu katika utandawazi‘ ;-Mwita Waitara
‘Bunge limeelekezwa na Serikali na Serikali imeingilia uhuru wa unge, kwahiyo hili bunge hapa lilipo halina meno‘ ;-Mwita Waitara
0 comments:
Post a Comment