Daladala zinazofanya safari zake katikati ya jiji zimetakiwa kuondoka ifikapo Mei
Hayo yameelezwa leo na Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (Dart),
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar
es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk. Amelisema tayari wamiliki wote wa
mabasi walishalipwa fidia ya kubadili njia.
“Wamiliki wote wa mabasi wameshalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka
jana, hakuna anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabara kabla ya
Mei 10,” amesema Mabrouk.
Mradi wa Dart unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu na tayari mabasi
hayo yameshaanza kufanya majaribio katika njia mbali mbali katikati ya
jiji huku changamoto kubwa ikidaiwa na waendesha pikipiki, raia na
daladala kupita kwenye njia hiyo ya mradi na kusababisha msongamano wa
magari kitendo ambacho kinalazimu mabasi hayo nayo kujikuta yakikaa
foleni

0 comments:
Post a Comment