Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika Hotuba yake ambayo pia
alitengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela
ambaye alikubali kutoa taarifa ambazo si sahihi kuwa Mkoa wa Shinyanga
hauna watumishi hewa, japo katika uhakiki uliofanyika mara baada ya
taarifa hiyo kumebainika kuwa kuna zaidi ya watumishi 45 ambao ni hewa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli amesema
amewatuma watu kuwarekodi mawaziri ambao wamesikika wakilalamika
'chinichini' kukatwa kwa fedha za matumizi mengineyo ( OC- Other Charges
) katika bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha.
"Mawaziri
wengine nasikia wanalalamika kweli,sasa nimetuma watu kuwarekodi kwa
sababu mind set (fikra) zao bado hazijabadilika,wanafikiri watu bado
tupo kwenye trend hiyo hiyo,wasomi ni wengi,unaweza ukawateua leo na kesho ukawabadilisha, ili mradi twende kwenye trend ninayoitaka," alisema Magufuli.
Rais
Magufuli aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati
akizungumzia hatua ya bunge kubana matumizi na kuwezesha kupatikana kwa
kiasi cha shilingi bilioni 6 ambazo zitaelekezwa kwenye utengenezaji wa
madawati.
“Chief Secretary(Katibu Mkuu Kiongozi ), huo ndio muelekeo kwa Makatibu Wakuu, waache kudai OC… Nawasikia watu wanadai eti OC ni kidogo. Wakiona hazitoshi basi waache kazi, maana wenzao wabunge wamesema ni nyingi na wamebana matumizi," alisema Rais Magufuli na kuongeza:
0 comments:
Post a Comment