Na MUSA MATEJA, Risasi MCHANGANYIKODAR ES SALAAM: Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amekwaa skendo ya kudaiwa kumsaliti mpenzi wake, Moses Iyobo na kuchepuka na jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Mula.
Chanzo kilicho karibu na mwigizaji huyo kimevujisha ubuyu kuwa, Aunt amekuwa akimsaliti Iyobo kwa muda mrefu lakini amelifanya jambo hilo kuwa siri.
“Aunt mjanja amekuwa akichepuka lakini kwa siri sana, wanazurura katika viwanja mbalimbali na huyo jamaa lakini huwezi amini wanakuwa makini kweli hakuna mtu anayeweza kuwajua.
“Wanahakikisha jamaa anakuwa na wenzake ili asiweze kujulikana kirahisi. Ukiwaona wanakula bata unawaona kama ni kampani moja lakini wenyewe wanajua nini wanafanya,” kilisema chanzo chetu.
Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilimtumia picha mwanahabari wetu zinazo muonesha Aunt akiwa na jamaa huyo katika pozi linaloashiria wana urafiki uliopitiliza……
0 comments:
Post a Comment