
Mshtuko! Mwanafunzi wa wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mchikichini ‘B’ ya mjini hapa, Anosisye Gidion (12), ameacha viulizo kibao baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge cha mama yake, Judith Kilalu ‘Mama Kapipi’.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, majira ya saa 1:00 asubuhi nyumbani kwao maeneo ya Mji Mpya mjini hapa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Ashura na rafiki wa marehemu, Hussein walisema kuwa chanzo cha denti huyo kujinyonga kilidaiwa kuwa ni kitendo cha mama yake kumchapa na kumtishia kumpeleka polisi baada ya kuchukizwa na kitendo chake cha kurudi nyumbani saa 6:00 usiku huku akidaiwa kuonekana akiwa na kundi haramu la vibaka la Kizazi Jeuri.
![]() |
| Kanga Aliyotumia Kujinyongea |

0 comments:
Post a Comment