| Raisi John Magufuli |
umma zikiongozwa na watumishi wanaokaimu.
Hali hiyo inatokana na mahitaji ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009 zinazotaka nafasi zote zinazokaimiwa zizibwe ndani ya miezi sita, jambo ambalo litazipa kazi ya ziada mamlaka za uteuzi kutafuta watu wa kuziba nafasi zinazoachwa baada ya mtumishi ‘kutumbuliwa’.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (Tughe) cha Mkoa wa Temeke, Mwanaidi Shomari alisema inatakiwa nafasi zilizoachwa wazi zizibwe mapema kwa kuwa zikichukua muda mrefu huathiri utendaji wa taasisi husika.
“Wapo baadhi ya wanaokaimu ambao huogopa kufanya uamuzi kwa kisingizio kwamba hawana mamlaka kamili. Jambo hili huchelewesha ratiba za matarajio yaliyopangwa kutekelezwa ndani ya muda husika, hivyo kuathiri uzalishaji wa sekta nyingine zinazotegemea ofisi hiyo,” alisema Mwanaidi.
Kwa mujibu wa kifungu D25 (3) cha kanuni hizo, mamlaka ya uteuzi itatakiwa kuhakikisha mchakato wa kumteua mtu mwenye cheo husika unakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita.
Mtaalamu wa masuala ya rasilimali watu, Baraka Elias alisema licha ya kwamba kuacha mtu akaimu muda mrefu hakuna madhara makubwa kwa taasisi, ni vyema utaratibu wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi izibwe haraka.
Alisema tofauti na taasisi za sekta nyingine, Serikali huchukua muda mrefu kutafuta mtumishi wa kuziba nafasi inayokuwa wazi kutokana na kuhusisha uchunguzi wa kina wa mtu anayeteuliwa kwa kuangalia uwezo, kujituma, weledi wake na uadilifu.
“Mfano mzuri ni (Mamlaka ya Mapato Tanzania) TRA ambako ili kumpata Kamishna Mkuu ni lazima achunguzwe sana kutokana na unyeti wa nafasi na taasisi yenyewe kwa taifa,” alisema.
Kwa hali ya kawaida, alisema ndani ya miezi sita inatakiwa mtu anayekaimu awe amethibitishwa baada ya kujiridhisha na utendaji kazi wake, lakini si lazima apatiwe nafasi hiyo kwa sababu mamlaka ya uteuzi inaweza kumtafuta mtu mwingine kuziba pengo hilo.
Ikumbukwe kuwa ndani ya miezi mitatu ya awali ya Serikali ya Awamu ya Tano (SA5), kuna vigogo wa juu wa taasisi 16 za umma ama wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili au uteuzi wao umetenguliwa.
Hii ina maana kuwa nafasi hizo zote kwa sasa, zikiwamo zile zenye zaidi ya miezi mitatu kama za TRA, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) zitatakiwa kujazwa kwa haraka ndani ya muda uliosalia ili kutovunja sheria.
Kifungu D31 (a) na (b) cha kanuni hizo kinaeleza taratibu ambazo Serikali inatakiwa kuzifuata wakati wa kuchuja na kuchunguza mtumishi anayekuwa anapewa cheo.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Dk Laurian Ndumbaro alikiri kuwa Serikali hutumia muda mrefu kuwatathmini wahusika ili kujiridhisha kama wanafaa kwa nafasi zinazokuwa wazi.
Alisema licha ya uthibitisho huo, kukosa sifa stahiki kwa baadhi ya makaimu, kutokuwapo kwa kumbukumbu sahihi za ajira na uthibitisho wa vikao vilivyopendekeza majina hayo pia huchangia kwa kiasi ucheleweshaji wa uteuzi.
“Licha ya sifa za kitaaluma, zipo sababu nyingine za kiutumishi. Mamlaka husika ni lazima zijiridhishe na utendaji, maadili na historia ya utumishi wa muhusika. Wanaokaimu nafasi mbalimbali ni wengi kuliko timu ya vetting (uthibitisho) ndiyo maana wapo watu wanaokaa muda mrefu kabla hawajathibitishwa,” alisema Dk Ndumbaro.
Kwenye taasisi na idara nyingi za Serikali, watumishi wengi wanakaimu kutokana na uhamisho, vifo, likizo na masomo, kustaafu, kufukuzwa au kushtakiwa kwa watendaji husika ili kufanya huduma ziendelee kutolewa kama kawaida.
Ili kupunguza hilo kwenye ofisi za Serikali, Dk Ndumbaro alisema wameandaa mkakati unaoshirikisha halmashauri zote nchini kwa kuzitaka kutekeleza hatua zote muhimu zinazowahusu.
Hata hivyo, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), halijapata kaimu mkurugenzi mpaka sasa baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu, Dk Ramadhani Dau kuteuliwa kuwa balozi.
Hata wakati taasisi nyingi zikiendelea kukaimiwa, baadhi ya wadau kuacha taasisi muda mrefu zikiwa na makaimu hasa nafasi za juu, kunasababisha madhara katika utendaji.
0 comments:
Post a Comment