Wakati msuguano mkubwa ukiwa umeibuka, Mbongo Fleva, Rehema Chalamila
‘Ray C’ akisukuma madongo kwa Magazeti Pendwa ya Global Publishers
kwamba yanamtungia uongo kuhusu hali yake ya kurejea kubwia unga akisema
hayuko hivyo kwa sasa, kuna taarifa kwamba, Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho
Kikwete ‘JK’ amemuonya kuhusu kutozingatia matumizi ya dawa za
methadone.
Methadone ni dawa zinazotumiwa na waathirika wa matumizi ya madawa ya
kulevya ‘unga’ ambapo Ray C anatumia kwenye Hospitali ya Mwananyamala,
Dar baada ya kuathirika.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini hospitalini hapo, Ray C alipata onyo
hilo baada ya Magazeti ya Global kuandika kwamba nyota huyo amerejea
kwenye kubwia unga huku akiendelea na methadone, hali ‘inayomzimisha’
mara kwa mara.
“Jamani nataka kuwaambia, mnajua mlipoandika kwamba Ray C karejea kwenye
unga wakati akiendelea kutumia methadone, JK alisoma, akamtumia ujumbe
akimtaka ajiangalie kwenye kukazana kutumia dawa na kuachana moja kwa
moja na matumizi ya unga.
“JK amemtaka aangalie mwenendo wake kwa sasa. Yaani bwana sijui vipi, JK anamtakia mema lakini yeye hajijui tu.
“Lakini kubwa kuliko yote ni kwamba juzikati Ray C alikuja pale
Hospitali ya Mwananyamala (jijini Dar), akawaangukia madaktari wake
wanaomtibu akiwaomba msamaha kwamba amekuwa akiwapuuza katika ushauri
lakini amegundua wao ndiyo msaada mkubwa kwake,” kilisema chanzo hicho.
Kitendo hicho kinatokana na madaktari hao siku za karibuni kumshindwa
staa huyo katika kumpa mwongozo wa matumizi ya dawa hizo, hivyo kuamua
kumrudisha nyumbani kwao, Bunju, Dar
Taarifa zaidi zinasema kuwa pia baada ya Magazeti ya Global kuandika
habari ya anayemmaliza Ray C ni kijana Frank, ndugu zake wamemfuata na
kumrudisha nyumbani kwao, Arusha.
“Unajua ndugu zake walikuwa wakimtafuta, alipotoka kwenye gazeti wakamwona, wakamfuata Mwananyamala kumchukua,” kilisema chanzo.
Utafiti uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa ile ‘posti’ ya Ray C
aliyoitupia kwenye mtandao wake wa Instagram mara baada ya kuandikwa na
Gazeti la Ijumaa Wikienda la Machi 28, mwaka huu, habari ikiwa na
kichwa; RAY C ANASWA AMEZIMIKA, akitoa shutuma nzito kwamba picha zile
si zake bali ziliungwaungwa, ameifuta!
Udadisi zaidi unasema kuwa kufutwa kwa posti hiyo kunatokana na Mbongo
Fleva huyo kuguswa na dhamira yake huku pia michango ya wafuasi wake
waliojitokeza kumwandikia ukweli kumwambia, picha zile ni yeye na hakuna
aliyeziunga!
Ray C alipotafutwa juzi ili kujibu madai hayo alikosekana hewani licha ya kupigiwa simu mara kwa mara kwa siku nzima.
Chanzo:Global Publishers
0 comments:
Post a Comment