
Zimesambaa taarifa na picha kadhaa kuhusu gari la mwigizaji wa bongo movie Aunty Ezekiel kushikiliwa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na kwamba linatakiwa kulipiwa kodi lasivyo litaingizwa kwenye magari yatayouzwa kwa mnada, baada ya hiyo millardayo.com imempata Aunty Ezekiel kwenye Exclusive.
“Ukweli ni kwamba nilinunua ile gari kutoka South Africa na lililetwa na kaka yangu hivyo kabla sijalilipia ushuru ndio likakamatwa, yaani ilikuwa kabla ya kujua taratibu za kulipa ushuru ila kwa sasa nimeshazijua na nipo mbioni kuitoa, nilikamatwa siku nikienda kwenye birthday party ya Idriss.” >>> Aunty Ezekiel
0 comments:
Post a Comment