Wednesday, 16 March 2016

VIDEO: Rais Magufuli kayatoa masaa 360 ya kuwashughulikia wanaolipwa mishahara hewa

March 15 2016 wakuu wapya wa mikoa nchini walikuwa wakiapisha Ikulu, Dar es salaam. Licha ya kuwa ndio kwanza wamepewa viapo, lakini Rais John Pombe Magufuli amewaagiza wakuu hao wa Mikoa kuhakikisha ndani ya siku 15 wamesimamia kuwaondoa wafanyakazi hewa na mishahara hewa huku pia akisisitiza kuwakamata na kuwawajibishwa vijana wote wanaoshinda vijiweni bila kufanya kazi.
Wapo watu ambao wanalipwa mishahara na wamestaafu, wapo watu wamefungwa lakini wanalipwa mishahara, kila mwezi tunapoteza zaidi ya bilioni 2 za mishahara hewa
Wakurugenzi wahakikishe ndani ya siku 15 wafanyakazi hewa wote wawe wametolewa katika halmashauri zao, bila hivyo tukigundua kunawafanyakazi wamelipwa mishahara hewa basi wajihesabu hawana kazi tena
Kuhusu watu wasiofanya kazi na kushinda vijiweni? ‘Haiwezekani katika nchi hii vijana wanacheza Pool huku wazee wakiwa mashambani wakifanya kazi, kama hawawezi kufanya kazi kwa kuambiwa basi wafanye kazi kwa lazima
kwasababu kama amezoea kila siku ni kucheza shika pelekeni wakalime kwa nguvu, akitoka atatambua kuwa aiyefanya kazi na asilie, sitaki kusikia kuna mkoa unalalamika njaa
Unaweza kutazama hii video hapa chini kuipata full stori ilivyo

0 comments:

Post a Comment